Afrika Yangu


Nimezaliwa Afrika, naipenda Afrika na naitakia mema Afrika. Leo nimeamua kuperuzi kuhusu bara langu na haya ndiyo niliyokumbana nayo.

Afrika ni sehemu inayovutia sana na ni bara lenye utofauti mkubwa duniani. Ni nyumbani kwa watu wa aina tofauti, wanyama, hali ya hewa na maeneo ya kuvutia. Ni bara linalojulikana kwa mavazi yake mazuri ya rangi na historia ya kazi nzuri ya sanaa. Afrika ni mahali ambapo binadamu wa kwanza alionekana dunani.

Watu wa Afrika

Graca Machelni ni mwanamke pekee duniani aliyewahi kuwa mke wa Rais wa nchi mbili tofauti Afrika Kusini na Msumbiji

Bara la Afrika ni la pili duniani kwa idadi kubwa ya watu. Watu bilioni moja na ushee.
 
Watu wa Afrika wanaongea zaidi ya lugha elfu moja, baadhi ya makadirio yanaweka hii namba karibu na elfu mbili.
 
Dini kubwa Afrika ni Uislamu ikifuatiwa na Ukristo.
 
Watu wa Afrika wana idadi ya wastani wa asilimia 14.72 ya idadi ya watu duniani (Taarifa: Umoja wa Mataifa 2009)

Kuna watu wengi wanaongea kifaransa Afrika kuliko nchini Ufaransa. 
 
Mabaki ya binadamu mkongwe yaligundulika Ethiopia, yana takribani umri wa miaka 200,000.

Watu wa San kutoka Afrika Kusini mpaka leo bado wanatumia zana zilizokutwa mapangoni kutoke miaka 44,000 iliyopita.

Wanariadha wengi wa mbio za kasi duniani wanatoka kwenye kabila moja la Kalenjins kutoka Kenya.

Rais wa kwanza wa Zimbabwe alikuwa anaitwa Rais Banana.

Mfumo wa ardhi Afrika

Mto mrefu duniani upo barani Afrika, Nile wenye urefu wa maili 4,132.

Afrika ina jagwa kubwa duniani, Sahara ambalo lina ukubwa takribani sawa na Marekani.

Victoria falls ni maporomoko makubwa ya maji barani Afrika; lina urefu wa 355ft na upana wa maili moja.

Mlima Kilimanyaro (Tanzania) ni mlima mrefu barani Afrika na wapili kwa urefu duniani, 19,300ft. Mlima huu ni mrefu sana kana kwamba barafu inapatikana kileleni kwake japokua mlima upo karibu na ikweta.

Madagaska ndicho kisiwa kikubwa Afrika na kisiwa cha nne kwa ukubwa duniani. Kisiwa kipo Bahari ya Hindi kwenye pwani ya Afrika Mashariki.

Bara

Afrika ni bara la pili kwa ukubwa duniani, lenye eneo la mraba takribani maili 117M. Kwa namna nyingine Afrika ni kubwa kuliko China, Marekani, Mexiko, India na sehemu kubwa ya bara la ulaya likijumliswa.


Bara la ulaya na Afrika zinatenganishwa na Kilometa 14.3 tu za bahari na kuna maungeza ya kutengeneza daraja refu duniani.

Afrika ni bara lenye joto kuliko yote duniani.

Sudani ndiyo nchi kubwa Afrika, eneo la mraba wa maili 968.000.

Kairo ndio mji mkubwa Afrika.

Afrika imekatwa na ikweta. 


Wanyama

Mnyama wa ardhini mkubwa duniani, ni tembo wa Afrika.

Mnyama mrefu duniani,ni Twiga, Anaishi Afrika.

Mnyama wa ardhini mwenye kasi duniani ni Duma. Anaishi Afrika

Afrika ni nyumbani kwa reptile mkubwa duniani, Mamba wa Nile.

Gorila anayeweza kukutwa kwenye misitu ya bara la Afrika, ndiye Nyani mkubwa duniani.


Marais Watano Tajiri Barani Afrika


Nguvu duniani huleta umaarufu na pia utajiri. Wakuuu wa Nchi au Serikali wanatakiwa kuwa watumishi wa watu, ila hii kazi inaweza kuwa ngumu na isiyokuwa na shukrani. Watumishi wanapaswa kuwa na upendo wa kweli na Nchi yao kutekeleza majukumu hayo.


Watumishi halisi wanapaswa kuwa wamoja na watu wao na lazima kujua hisia za mtu wa kawaida. 
Rais mstaafu wa Urugwai Jose Mujica anapendwa sana kwa kutokujali nguvu alizonazo na kuamua kuishi uraiani na watu wakawaidi wa Urugwai. Wakati mwingine ni vyema kuwa tajiri kwa sababu itamruhusu mtumishi kufikisha lengo la kazi yake bila hofu ya fedha za kuangalia familia yake. Na fedha zinawasumbua sana wakuu wengi wa nchi, Hawa ni Vioungozi watano wa Afrika wenye pochi nene.

Paul Biya –Thamani $200M (Tsh 461b)
Nchi: Kameruni. Miaka ya uongozi: 32

Paul Biya amekuwa Rais wa Kameruni tungu 6-11-1982. Thamani yake inakadiriwa kufikia $200M. Mwaka 2009 Tovuti ya gazeti la RU 89 lilitoa taarifa ya kwamba mapumziko ya Rais wa Kameruni ndiyo makubwa kuliko rais yeyote yule duniani. Inasemekana anatumia $40,000 kwa siku kukodisha ‘villa’




Uhuru Kenyatta- Thamani $500M (Tsh 1.2 Trillion)
Nchi: Kenya, Miaka ya uongozi: 2



Uhuru MUIGAI Kenyatta ni Rai wa Kenya na mwana wa Rais wa kwanza wa Kenya, Jomo Kenyatta. Mwaka 2011, ‘Forbes’ ilikadiria thamani yake kuwa dola milioni 500. Mali yake nyingi inatokana na majengo na familia yake Rais anamiliki hisa kwenye kampuni kubwa ya maziwa ya nchini kenya ‘Brookside Dairies’ chombo cha habari Mmediamax, Heritage Hotels, Commercial Bank of Africa na mamia ya elfu ya ardhi kuu nchini Kenya. 



Teodoro Obiang Nguema Mbasogo – Thamani $600M (Tsh 1.4 Trillion)
Nchi: Guinea ya Ikweta , Miaka ya Uongozi: 34

Teodoro Obiang Nguema Mbasogo ni Rais wa Guinea ya Ikweta . Aliingia madarakani mwezi Agosti 1979 kwa kumpindua mjomba wake Francisco Macias Nguema katika mapinduzi ya kijeshi. Amesimamia mafuta kwenye nchi hiyo toka mwaka 1990. Kwa kifupi Rais na familia yake wanamiliki uchumi wa Nchi. Kwa mujibu wa ‘Forbes’ 2006 ilisemekana ana $600M. Mwaka 2011 Serikali ya Marekani walikamata mali zenye thamani ya $70M za mwanae Teodoro Nguema Obiang Mangue(42) ambeye pia ni Makamo wa pili wa Rais.. Japokuwa Guine ni nchi ya pili kwa utajiri barani Afrika, idadi kubwa ya watu wanaishi chini ya mstari wa umasikini.


Mohammed VI - Thamani : $2.1B (Tsh. 6,916,500,000,000.00 T)
Nchi: Morocco, Miaka ya uongozi: 15

Mohammed VI ni Mfalme wa Morocco. Na pia ni mfanya biashara anayeongoza nchi kwake. Kwa mujibu wa ‘Forbes’ ana thamani zaidi ya $2.5B. Mfalme alipata taji lake baada ya baba yake kufariki 1999 na mara mojo kuboresha rekodi yake mbaya dhidi ya haki za binadamu na kupunguza umasikini.

Jose Eduardo dos Santos - Thamani:$20b (Tsh. 46,110,000,000,000.00t)
Nchi: Angola, Miaka ya uongozi: 35



Jose Eduardo dos Santos ni Rais wa Angola. Ameka kwenye kiti hicho tangu 1979. Wakati asilimi 70 ya Waangola wanaishi chini ya dola mbili (Tsh500) kwa siku. Mwanae Isabel dos Santos ni mmoja kati ya Mabilionea wa Afrika na thamani ya £3.8b. Kwa sasa ni mwanamke tajiri Afrika na mwanake tajiri mweui dunia nzima.

HUDUMA YA 'DRY CLEANING AND LAUNDRY' AFRIKA


JINSI YA KUANZISHA BIASHARA INAYOTENGENEZA FEDHA KUTOKANA NA MAVAZI MACHAFU
BARANI AFRIKA



Ufuaji wa nguo zetu ni moja ya kazi nyingi tunazozichukia. Kila mtu anataka kuvaa nguo safi na zilizopigwa pasi vizuri, ila hakuna mtu anayependa kufua na kupiga pasi hususani kwa mikono. Maisha ya mjini yanachukua muda mwingi sana wa watu wakifanywa kazi hivyo kuwafanya watu wengi zaidi kuwa tayari kulipia kufulia na kupigiwa pasi nguo zao chafu.
Soko la biashara ya 'dry cleaning and laundry' ni nono sana Afrika na linaongezeka kwa kiwango kikubwa. Biashara hii inaweza kufanyika kutoka nyumbani kwa mtaji mdogo tu wa uwekezaji. Ni mgodi wa dhahabu kwa wajasiriamali wenye upeo wanoweza kutoa urahisi unahoitajiwa na wateja kwa bei ya kuridhisha. Makala hii inahusu biashara hii ya kuvutia na jinsi unavyoweza kuianza au kuifanywa.

Kumbuka: Hapa naongelea ‘Dry cleaning and Laundry’. ‘Dry cleaning’ ni jinsi ya kusafisha nguo kwa kutumia kemikali maalumu (si maji).  ‘Dry cleaning’ inahitaji ujuzi wa kiufundi na inafaa wakatai nguo zinafuliwa ni tete na haziwezi kuhimili kufuliwa kwa mkono au mashine ya kawaida.

‘ Laundry’ Ni kufua kwa ujumla, inahusisha matumizi ya maji, sabuni ya unga au sabuni ya maji kusafisha nguo.

Kwa nini soko la huduma ya ‘Dry cleaning and laundry’  linaongezeka barani Afrika?
  • Waafrika wengi wanaishi mijini

Jinsi maisha ya mjini yalivyo, yanachangia sana mahitaji ya kupanda huduma za kurahisisha maisha kama ‘dry cleaning and laundry’.  Watu huwa ‘busy’ sana wakifanya kazi 9-5 au wengine kuendesha biashara zao wenyewe mara nyingi wakirejea nyumbani wanakuwa hoi na uchovu juu na ni vigumu kupata muda wa kuhangaika na nguo zao. Mwisho wa wiki siku hizi watu bora wapumzike kwa utulivu baada ya kufanya kazi kwa bidii wiki nzima au watoke wakaburudishe miyoo yao na watu wengi hawapo tayiri kuuachi muda wao wakupumua wakati wao wa mapumziko kufua nguo. 

Kuna nafasi gani kwa wajasiriamali barani Afrika kwenye soko la ‘dry cleaning and laudry’


Jambo linavutia kuhusu soko la huduma ya ‘dry cleaning and laundry’ Afrika ni kwamba kila mmoja, ikiwa ni pamoja na matajiri na wasio matajiri wapo tayari kulimpa mtu mwingine awafulie nguo zao. Kutoka na soko unalotaka kulenga, kumudu bei itakuwa sababu kubwa kwa baadhi ya wateja kwenye vitongoji masikini. Wakati ubora wa huduma na urahisi wa kuwafikia wengine huduma itakuwa ni sababu kuu ya uamuzi wa kutumia huduma yako kwa wengine. 

Tutaangalia aina chache za fursa zinazoweka kutumika katika soko hili ili kujenga biashara yenye faidi kubwa.

Huduma ya kuchukua na kurejesha


Kwa watu wengi jijini siyo tu kuhusu kupata mtu mwingine kuwafulia nguo zao, kinachowakabili ni muda. Masaa ya kazi yanawabana watu, kupeleka mavazi dukani kwa waoshaji na kuri siku kadhaa kuzichukua inawawia watu wengi vigumu. Watu wengi watapendelea mtu kuja nyumbani au ofisini kwao kuchukua mavazi na kurejesha yakiwa tayari. Na hii sehemu ya soko amabayo watu wapo tayari kulipia huduma hii ziada na wataifurahia sana.

Watu wenye uwezekano wa kusaini huduma hii ni wanataaluma walipo ‘busy’ sana na kazi na wanaokabiliwa na masaa marefu ya kazi wiki nzima na kutumia muda wao mwingi kwenye foleni. Wana haja ya kuonekana watanashati kazini ila inawahia vigumu kwa kutokuwa na muda na uchovu.


Wajasiriamali wwenye nia na sehemu hii ya soko, wanaweza kuwekeza kwenye vifaa vya kufulia wenyewe au kuwapatia maduka yanayofanya kazi za ufuaji. Faida unyotengeneza  ni tofauti kati ya kiasi uchowalipa wafuaji na malipo unayochukua kutoka kwa wateja wako.

Faidi kutokana na biashara hii inaweza kuwa kubwa kama wateja wako ni wanataaluma tajiri ambao wanakipa kipaumbele cha juu ubora wa huduma yako na urahisi unaowapatia kwa kiasi wanacholipa.

Fungua duka la 'cleaning and laundry'

Duka la ufuaji ‘laundry shop’ ni mahali ambapo upangaji, uoshaji, ukashaji na upigaji pasi (pressing) vinafanyika. Wajasiriamali wanaendesha hii biashra kutoka nyumbani au kwenye sehemu ndogo huwa wanatumia njia mwongozo, kama uoshaji kwa mikono. Kutokana na uhaba mkubwa wa ajira katika maeneo mengi ya Afrika, ni rahisi kupata wahudumu nafuu kukufanyia kazi.
Hili chaguo mwongozo linahitaji kiasi kidogo cha kuanzia na bei ya kuendesha huduma ipo chini. Aini hii ya huduma itawarufaa wateja wanaojarli kuhusu bei na watalipa ada ya chini kwa ajili ya huduma ya kufua. 

Wakati mbinu mwongozo itafanikiwa na wateje wachache, idadi ya wateje inapoongezeka gharama itakuwa nafuu ukiwekeza kwenye mashine sahihi za kufulia. Mashine za kufuli zinakuja kwa ukubwa mbalimbali na hupimwa kulingana na uzito wa nguo zinazoweza kuhimili. Mashine inawastani wa kufanya kazi kwa miaka 15 kulingana na ubora na matumizi.

Kama unakusudia kuanzisha biashara ya ‘laundry and dry cleaning deliver’ kuopoa na kurejesha pekee. Uwekezaji wako mkubwa utakuwa kwenye gari la kubebea mavazi. Mavazi safi yanahitaji kuning’ing’inizwa kwenye ‘racks’ ndani ya gari wakati wa kuzirejesha kepusha mikunjo.


Tangu biashara nzima inategemea gari, ni muhimu kuhakikisha linahimarisha na kuangaliwa vizuri wakati wote. Pia itakuwa muhimu kuwa na mpango wa kukabiliana na uharibifu na matatizo ya mitambo. 

Hata hivyo, kama unaanzisha duka la ‘dry cleaning and laundry', mataji zaidi yatahitajika, kulipia kodi, huduma (umeme na maji), bidhaa za matumizi (sabuni za unga, sabuni za maji, kemikali nk).
Tangu wateja wengi hawalipii huduma mpaka mavazi yao yanaporudishwa safi, itabidi kuhifadhi pembene baadhi ya mtaji ili kuwalipa wafanya kazi wako na gharama nyingine tangu ndio kwanza biashara changa.

Huduma kwa wateja inaweza ikakujenga au ikakubomoa

Dunia kote mteja ni mfalme, kama ukiwahudumia wateja wako vizuri, uwezekano wa wao kutumia huduma yako ni mkubwa na wanaweza kukupendekeza kwa ndugu, jamaa na marafiki. Hasa kwa ajili ya huduma ya kuchukua na kurejesha. Ni muhimu kuchukua na kurejea mavazi kwa wakati na kuhakikisha mavazi masafi kama dheruji. Unaweza pia kutoa mifuko yako ya nguo kwa wateja wako. Hii mifuko inaweza kuwa na jina la kampuni yako, nambari ya simu na anwani ya tovuti zilizochapishwa juu yake. Hii mifuko inaweza kutumika kama chombo cha kutangaza soko lako.
Kwenye hii biashara migogoro inaweza kutoka na mara nyingi inaweza kusababisha matatizo.  Kabla ya kukubali mavazi yaliyokuwa na madoa mazito inapaswa kuongea na mteja wako na kumfahamisha kwamba hakuna uhakika wa asilimi 100 kwamba madoa yatatoka kabisa.

Eneo

Kama unampango wakuanza biashara ya kusafisha na kusafirisha mavazi ya wateja wako, eneo halijalishi sana tangu utakuwa unakutana na wateje wako kuchukua na kurejesha mavazi yao. Hata hivyo kama umbali kati ya wateja wako na ‘dry cleaner and laundry’ ni mbali sana, unaweza kutumia fedha nyingi kwenye mafuta ya gari la kurejeshea mavazi. Ni vizuri kukubaliana na wateja siku utakayokwenda kuchukua mavazi yao. Kwa njia hii, unajipanga vizuri na unapangiria njia yako ya kuzunguruka mjini kwa umakini.

Kama utaka kuendesha biashara ya kufua tu bila kuchukua na kurejesha mavazi ya wateja wako, haitajalisha duka lako lilipo. Ila unaweza kuhitaji kufungua kituo cha ukusanyaji katika eneo kuu lilo karibu na wateja wako.

Gharama unazohitaji kuangalia

Kutokana na uhaba wa umeme katika miji mingi ya Afrika. Biashara nyingi hazina budi ila kumiliki majenereta.Japokuwa gharama hizi za kutumia jenereta haifanyi biashara isipate faida, ni muhimu kuiweka kichawani daima.

Gharama nyingi ni wafanya kazi. Kama unatumia mashine basi utakuwa na wafanyakazi wachache.

Kiasi cha malipo

Bei ya malipo itatokana na huduma yako, itategemea na kiasi gani wateja wako wanaweza kumudu na thamani ya huduma yako. Fanya utafiti kujua ni kiasi gani wengine wanalipisha kwa huduma hiyo. Fanya utafiti wa haraka wa soko na kujua kama wanaridhiswa na huduma iliyopo. Je nini malalamiko yao, bei kubwa mno, huduma mbovu kwa wateja, ucheleweshwaji wa kuchukuaa na kurejesha mavazi n.k.

Soko la ‘dry cleaning and laundry’ Afrika lipo kwenye njia ya ukuaji wa kutosha. Watu zaidi wahaja ya hii huduma ili kurahisha maisha yao ambayo yako ‘busy’ sana. Tangu karibia kila mtu hapendi kufua nguo zao wenyewe, wajasiriamali wanaweza kuchonga njia mbadala itakayowapatia faida kubwa na mafaniko kwenye hii biashara.