Afrika Yangu


Nimezaliwa Afrika, naipenda Afrika na naitakia mema Afrika. Leo nimeamua kuperuzi kuhusu bara langu na haya ndiyo niliyokumbana nayo.

Afrika ni sehemu inayovutia sana na ni bara lenye utofauti mkubwa duniani. Ni nyumbani kwa watu wa aina tofauti, wanyama, hali ya hewa na maeneo ya kuvutia. Ni bara linalojulikana kwa mavazi yake mazuri ya rangi na historia ya kazi nzuri ya sanaa. Afrika ni mahali ambapo binadamu wa kwanza alionekana dunani.

Watu wa Afrika

Graca Machelni ni mwanamke pekee duniani aliyewahi kuwa mke wa Rais wa nchi mbili tofauti Afrika Kusini na Msumbiji

Bara la Afrika ni la pili duniani kwa idadi kubwa ya watu. Watu bilioni moja na ushee.
 
Watu wa Afrika wanaongea zaidi ya lugha elfu moja, baadhi ya makadirio yanaweka hii namba karibu na elfu mbili.
 
Dini kubwa Afrika ni Uislamu ikifuatiwa na Ukristo.
 
Watu wa Afrika wana idadi ya wastani wa asilimia 14.72 ya idadi ya watu duniani (Taarifa: Umoja wa Mataifa 2009)

Kuna watu wengi wanaongea kifaransa Afrika kuliko nchini Ufaransa. 
 
Mabaki ya binadamu mkongwe yaligundulika Ethiopia, yana takribani umri wa miaka 200,000.

Watu wa San kutoka Afrika Kusini mpaka leo bado wanatumia zana zilizokutwa mapangoni kutoke miaka 44,000 iliyopita.

Wanariadha wengi wa mbio za kasi duniani wanatoka kwenye kabila moja la Kalenjins kutoka Kenya.

Rais wa kwanza wa Zimbabwe alikuwa anaitwa Rais Banana.

Mfumo wa ardhi Afrika

Mto mrefu duniani upo barani Afrika, Nile wenye urefu wa maili 4,132.

Afrika ina jagwa kubwa duniani, Sahara ambalo lina ukubwa takribani sawa na Marekani.

Victoria falls ni maporomoko makubwa ya maji barani Afrika; lina urefu wa 355ft na upana wa maili moja.

Mlima Kilimanyaro (Tanzania) ni mlima mrefu barani Afrika na wapili kwa urefu duniani, 19,300ft. Mlima huu ni mrefu sana kana kwamba barafu inapatikana kileleni kwake japokua mlima upo karibu na ikweta.

Madagaska ndicho kisiwa kikubwa Afrika na kisiwa cha nne kwa ukubwa duniani. Kisiwa kipo Bahari ya Hindi kwenye pwani ya Afrika Mashariki.

Bara

Afrika ni bara la pili kwa ukubwa duniani, lenye eneo la mraba takribani maili 117M. Kwa namna nyingine Afrika ni kubwa kuliko China, Marekani, Mexiko, India na sehemu kubwa ya bara la ulaya likijumliswa.


Bara la ulaya na Afrika zinatenganishwa na Kilometa 14.3 tu za bahari na kuna maungeza ya kutengeneza daraja refu duniani.

Afrika ni bara lenye joto kuliko yote duniani.

Sudani ndiyo nchi kubwa Afrika, eneo la mraba wa maili 968.000.

Kairo ndio mji mkubwa Afrika.

Afrika imekatwa na ikweta. 


Wanyama

Mnyama wa ardhini mkubwa duniani, ni tembo wa Afrika.

Mnyama mrefu duniani,ni Twiga, Anaishi Afrika.

Mnyama wa ardhini mwenye kasi duniani ni Duma. Anaishi Afrika

Afrika ni nyumbani kwa reptile mkubwa duniani, Mamba wa Nile.

Gorila anayeweza kukutwa kwenye misitu ya bara la Afrika, ndiye Nyani mkubwa duniani.


1 comment:

  1. Our EcoDrive Titanium Watch - iTanium Arts
    This stylish, full-on titanium watch allows you to set out does titanium set off metal detectors to babyliss nano titanium flat iron create a titanium earring posts lifestyle titanium app of comfort. Watch the action on titanium paint color your own home screen from your personal

    ReplyDelete