JINSI YA KUANZISHA BIASHARA INAYOTENGENEZA FEDHA KUTOKANA NA MAVAZI MACHAFU
BARANI AFRIKA
Ufuaji wa nguo zetu ni moja ya kazi nyingi tunazozichukia.
Kila mtu anataka kuvaa nguo safi na zilizopigwa pasi vizuri, ila hakuna mtu
anayependa kufua na kupiga pasi hususani kwa mikono. Maisha ya mjini yanachukua muda mwingi sana wa watu wakifanywa kazi hivyo kuwafanya
watu wengi zaidi kuwa tayari kulipia kufulia na kupigiwa pasi nguo zao chafu.
Soko la biashara ya 'dry cleaning and laundry' ni nono sana Afrika na linaongezeka kwa kiwango kikubwa. Biashara hii inaweza kufanyika kutoka nyumbani kwa mtaji mdogo tu wa uwekezaji. Ni mgodi wa dhahabu kwa wajasiriamali wenye upeo wanoweza kutoa urahisi unahoitajiwa na wateja kwa bei ya kuridhisha. Makala hii inahusu biashara hii ya kuvutia na jinsi unavyoweza kuianza au kuifanywa.
Soko la biashara ya 'dry cleaning and laundry' ni nono sana Afrika na linaongezeka kwa kiwango kikubwa. Biashara hii inaweza kufanyika kutoka nyumbani kwa mtaji mdogo tu wa uwekezaji. Ni mgodi wa dhahabu kwa wajasiriamali wenye upeo wanoweza kutoa urahisi unahoitajiwa na wateja kwa bei ya kuridhisha. Makala hii inahusu biashara hii ya kuvutia na jinsi unavyoweza kuianza au kuifanywa.
Kumbuka: Hapa naongelea ‘Dry cleaning and Laundry’. ‘Dry
cleaning’ ni jinsi ya kusafisha nguo kwa kutumia kemikali maalumu (si
maji). ‘Dry cleaning’ inahitaji ujuzi wa kiufundi na inafaa wakatai nguo zinafuliwa ni tete na haziwezi kuhimili kufuliwa kwa mkono au mashine ya kawaida.
‘ Laundry’ Ni kufua kwa ujumla, inahusisha matumizi ya maji, sabuni ya unga au sabuni ya maji kusafisha nguo.
‘ Laundry’ Ni kufua kwa ujumla, inahusisha matumizi ya maji, sabuni ya unga au sabuni ya maji kusafisha nguo.
Kwa nini soko la huduma ya ‘Dry cleaning and laundry’ linaongezeka barani Afrika?
- Waafrika wengi wanaishi mijini
Jinsi maisha ya mjini yalivyo, yanachangia sana mahitaji ya kupanda huduma za kurahisisha maisha kama ‘dry cleaning and laundry’. Watu huwa ‘busy’ sana wakifanya kazi 9-5 au
wengine kuendesha biashara zao wenyewe mara nyingi wakirejea nyumbani wanakuwa hoi na uchovu juu na ni vigumu kupata muda wa kuhangaika na nguo zao. Mwisho wa
wiki siku hizi watu bora wapumzike kwa utulivu baada ya kufanya kazi kwa bidii
wiki nzima au watoke wakaburudishe miyoo yao na watu wengi hawapo tayiri kuuachi muda wao wakupumua wakati wao wa mapumziko
kufua nguo.
Kuna nafasi gani kwa wajasiriamali barani Afrika kwenye soko
la ‘dry cleaning and laudry’?
Jambo linavutia kuhusu soko la huduma ya ‘dry cleaning and
laundry’ Afrika ni kwamba kila mmoja, ikiwa ni pamoja na matajiri na wasio
matajiri wapo tayari kulimpa mtu mwingine awafulie nguo zao. Kutoka na soko
unalotaka kulenga, kumudu bei itakuwa sababu kubwa kwa baadhi ya wateja kwenye
vitongoji masikini. Wakati ubora wa huduma na urahisi wa kuwafikia wengine huduma
itakuwa ni sababu kuu ya uamuzi wa kutumia huduma yako kwa wengine.
Tutaangalia aina chache za fursa zinazoweka kutumika katika soko hili ili kujenga biashara yenye faidi kubwa.
Huduma ya kuchukua na kurejesha
Kwa watu wengi jijini siyo tu kuhusu kupata mtu mwingine
kuwafulia nguo zao, kinachowakabili ni muda. Masaa ya kazi yanawabana watu, kupeleka mavazi dukani kwa waoshaji
na kuri siku kadhaa kuzichukua inawawia watu wengi vigumu. Watu wengi watapendelea mtu kuja nyumbani au ofisini kwao
kuchukua mavazi na kurejesha yakiwa tayari. Na hii sehemu ya soko amabayo watu wapo tayari
kulipia huduma hii ziada na wataifurahia sana.
Watu wenye uwezekano wa kusaini huduma hii ni
wanataaluma walipo ‘busy’ sana na kazi na wanaokabiliwa na masaa marefu ya kazi wiki
nzima na kutumia muda wao mwingi kwenye foleni. Wana haja ya kuonekana
watanashati kazini ila inawahia vigumu kwa kutokuwa na muda na uchovu.
Wajasiriamali wwenye nia na sehemu hii ya soko, wanaweza
kuwekeza kwenye vifaa vya kufulia wenyewe au kuwapatia maduka yanayofanya kazi za ufuaji. Faida unyotengeneza ni tofauti kati ya
kiasi uchowalipa wafuaji na malipo unayochukua kutoka kwa wateja wako.
Faidi kutokana na biashara hii inaweza kuwa kubwa kama wateja wako ni wanataaluma tajiri ambao wanakipa kipaumbele cha juu ubora wa huduma yako na urahisi unaowapatia kwa kiasi wanacholipa.
Faidi kutokana na biashara hii inaweza kuwa kubwa kama wateja wako ni wanataaluma tajiri ambao wanakipa kipaumbele cha juu ubora wa huduma yako na urahisi unaowapatia kwa kiasi wanacholipa.
Fungua duka la 'cleaning and laundry'
Duka la ufuaji ‘laundry shop’ ni mahali ambapo upangaji,
uoshaji, ukashaji na upigaji pasi (pressing) vinafanyika. Wajasiriamali wanaendesha hii biashra kutoka nyumbani au kwenye sehemu ndogo huwa wanatumia
njia mwongozo, kama uoshaji kwa mikono. Kutokana na uhaba mkubwa wa ajira
katika maeneo mengi ya Afrika, ni rahisi kupata wahudumu nafuu kukufanyia kazi.
Hili chaguo mwongozo linahitaji kiasi kidogo cha kuanzia na
bei ya kuendesha huduma ipo chini. Aini hii ya huduma itawarufaa wateja wanaojarli kuhusu bei na watalipa ada ya chini kwa ajili ya huduma ya kufua.
Kama unakusudia kuanzisha biashara ya ‘laundry and dry
cleaning deliver’ kuopoa na kurejesha pekee. Uwekezaji wako mkubwa utakuwa kwenye gari la kubebea mavazi. Mavazi safi yanahitaji kuning’ing’inizwa kwenye ‘racks’
ndani ya gari wakati wa kuzirejesha kepusha mikunjo.
Tangu biashara nzima inategemea gari, ni muhimu kuhakikisha linahimarisha na kuangaliwa vizuri wakati wote. Pia itakuwa muhimu kuwa na mpango wa kukabiliana na uharibifu na matatizo ya mitambo.
Hata hivyo, kama unaanzisha duka la ‘dry cleaning and
laundry', mataji zaidi yatahitajika, kulipia kodi, huduma (umeme na maji), bidhaa
za matumizi (sabuni za unga, sabuni za maji, kemikali nk).
Tangu wateja wengi hawalipii huduma mpaka mavazi yao yanaporudishwa safi, itabidi kuhifadhi pembene baadhi ya mtaji ili kuwalipa wafanya
kazi wako na gharama nyingine tangu ndio kwanza biashara changa.
Huduma kwa wateja inaweza ikakujenga au ikakubomoa
Dunia kote mteja ni mfalme, kama ukiwahudumia wateja wako vizuri, uwezekano wa wao
kutumia huduma yako ni mkubwa na wanaweza kukupendekeza kwa ndugu, jamaa na
marafiki. Hasa kwa ajili ya huduma ya kuchukua na kurejesha. Ni muhimu kuchukua na
kurejea mavazi kwa wakati na kuhakikisha mavazi masafi kama dheruji. Unaweza
pia kutoa mifuko yako ya nguo kwa wateja wako. Hii mifuko inaweza kuwa na jina
la kampuni yako, nambari ya simu na anwani ya tovuti zilizochapishwa juu yake.
Hii mifuko inaweza kutumika kama chombo cha kutangaza soko lako.
Kwenye hii biashara migogoro inaweza kutoka na mara nyingi
inaweza kusababisha matatizo. Kabla ya
kukubali mavazi yaliyokuwa na madoa mazito inapaswa kuongea na mteja wako na
kumfahamisha kwamba hakuna uhakika wa asilimi 100 kwamba madoa yatatoka kabisa.
Eneo
Kama unampango wakuanza biashara ya kusafisha na kusafirisha
mavazi ya wateja wako, eneo halijalishi sana tangu utakuwa unakutana na wateje
wako kuchukua na kurejesha mavazi yao. Hata hivyo kama umbali kati ya wateja wako
na ‘dry cleaner and laundry’ ni mbali sana, unaweza kutumia fedha nyingi kwenye
mafuta ya gari la kurejeshea mavazi. Ni vizuri kukubaliana na wateja siku utakayokwenda kuchukua mavazi yao. Kwa njia hii, unajipanga vizuri na
unapangiria njia yako ya kuzunguruka mjini kwa umakini.
Kama utaka kuendesha biashara ya kufua tu bila kuchukua na kurejesha mavazi ya wateja wako, haitajalisha duka lako lilipo. Ila unaweza kuhitaji kufungua kituo cha ukusanyaji katika eneo kuu lilo karibu na wateja wako.
Gharama unazohitaji kuangalia
Kutokana na uhaba wa umeme katika miji mingi ya Afrika.
Biashara nyingi hazina budi ila kumiliki majenereta.Japokuwa gharama hizi za
kutumia jenereta haifanyi biashara isipate faida, ni muhimu kuiweka kichawani
daima.
Gharama nyingi ni wafanya kazi. Kama unatumia mashine basi
utakuwa na wafanyakazi wachache.
Kiasi cha malipo
Bei ya malipo itatokana na huduma yako, itategemea na kiasi
gani wateja wako wanaweza kumudu na thamani ya huduma yako. Fanya utafiti kujua
ni kiasi gani wengine wanalipisha kwa huduma hiyo. Fanya utafiti wa haraka wa
soko na kujua kama wanaridhiswa na huduma iliyopo. Je nini malalamiko yao, bei
kubwa mno, huduma mbovu kwa wateja, ucheleweshwaji wa kuchukuaa na kurejesha
mavazi n.k.
Soko la ‘dry cleaning and laundry’ Afrika lipo kwenye njia
ya ukuaji wa kutosha. Watu zaidi wahaja ya hii huduma ili kurahisha maisha yao
ambayo yako ‘busy’ sana. Tangu karibia kila mtu hapendi kufua nguo zao
wenyewe, wajasiriamali wanaweza kuchonga njia mbadala
itakayowapatia faida kubwa na mafaniko kwenye hii biashara.
Nahitaji mashine hizi je nitazipataje.
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
DeleteNiandae mashine zp il niweze kufunga?
DeleteNahitaji kufaham mashine za kufulia aina, bei na ubora wake katika matumizi ya umeme
ReplyDeletesomo limekaa powa
ReplyDeletesomo limekaa powa
ReplyDeleteHello guys naweza kupata machine ya kufulia nguo chini ya 200,000/= nipo Moshi no Yangu ni 0764 175 653
ReplyDeletenice
ReplyDeleteNice
ReplyDeletesomo lime eleweka kama kuna mtu ana nyongeza juu ya jinsi yakupata wateja
ReplyDeleteAhsante umenisaidia sana kwa somo hili zuri
ReplyDeleteasante sana kwa wazo
ReplyDeleteNimeelewa lakini hujaweka kianzio cha mtaji sasa MTU kama anataka itajuwa
ReplyDeleteKuna mashine ya 200000 no 0675271358
ReplyDeleteTunashukuru kwa kutuelewesha vizuri
ReplyDeleteJe? nitajuaje ubora wa mashine na kampuni nzuri ni ipi?
ReplyDeleteNahitaji kujua machine nzuri ya kuwa nayo kwa matumizi ya nyumbani na Bei zake no yangu 0620480821
ReplyDelete